Thursday, August 25, 2016
RAIS MAGUFULI APOKEA TAARIFA YA UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA KUTOKA UGANDA HADI BANDARI YA TANGA
Do you like this story?
Makamu
wa Rais wa Kampuni ya Total Afrika Mashariki Bw. Javiero Rielo amemhakikishia
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwa
maandalizi ya kuanza kwa ujenzi wa bomba la mafuta la kutoka Hoima nchini
Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania yanaendelea vizuri na kwamba
kampuni hiyo imedhamiria kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kwa mafanikio.
Bw.
Javiero Rielo amesema hayo jana tarehe 24 Agosti, 2016 Ikulu Jijini Dar es
Salaam alipokutana na Rais Magufuli kwa lengo la kumpa taarifa juu ya maendeleo
ya maandalizi ya kuanza kwa ujenzi wa bomba la mafuta.
Mradi
huo utahusisha ujenzi wa bomba lenye urefu wa kilometa 1,410 ambalo
litasafirisha mafuta ghafi kutoka ziwa Albert nchini Uganda hadi Bandari ya
Tanga nchini Tanzania na unatarajiwa kuzalisha ajira za moja kwa moja 1,500 na
ajira zisizo za moja kwa moja 20,000.
Gharama
za mradi wa ujenzi wa bomba hilo zinatarajiwa kuwa takribani Dola za Kimarekani
Bilioni 4 na Kampuni ya Total inasema fedha hizo zipo tayari.
Akizungumza
baada ya kupokea taarifa hiyo, Rais Magufuli amesema anaamini kuwa mradi huo
utakuwa na manufaa makubwa kwa Tanzania, Uganda, Kampuni ya Total na nchi
jirani.
Amebainisha
kuwa pamoja na kwamba Tanzania ipo katika mazingira mazuri ya kutekeleza mradi
huo, Serikali yake itatoa ushirikiano mkubwa ili kufanikisha mradi huo.
Katika
hatua nyingine, Rais Magufuli amepokea hati za utambulisho kutoka kwa mabalozi
watatu wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini.
Mabalozi
waliowasilisha hati zao ni Mhe. Ian Myles – Balozi wa Canada hapa nchini, Mhe.
Prasittiporn Wetprasit – Balozi wa Thailand hapa nchini mwenye makazi yake
Mjini Nairobi nchini Kenya na Mhe. Harald Gunther – Balozi wa Austria hapa
nchini mwenye makazi yake Mjini Nairobi nchini Kenya.
Pamoja
na kuwasilisha hati zao za utambulisho Mabalozi hao wameelezea kufurahishwa na
mahusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati ya nchi zao na Tanzania na wameahidi
kufanya kazi bega kwa bega na Serikali ya Tanzania ili wananchi wa pande zote
wanufaike na matokeo ya ushirikiano huo hususani katika uwekezaji na biashara.
Kwa
upande wake Rais Magufuli amewahakikishia Mabalozi hao kuwa Serikali yake
itaendeleza na kukuza zaidi ushirikiano kati ya Tanzania na nchi hizo na ametoa
wito kwa Mabalozi hao kuzishawishi zaidi nchi zao na wawekezaji katika nchi
hizo kushirikiana na Tanzania katika ujenzi wa viwanda, uongezaji thamani ya
madini, kuendeleza kilimo hususani kilimo cha umwagiliaji, uzalishaji wa
nishati na biashara mbalimbali.
Pia
Rais Magufuli ametoa wito kwa Mabalozi wa Thailand na Austria kuanzisha ofisi
za Ubalozi hapa nchini ili kurahisisha na kuharakisha shughuli za kibalozi.
Gerson
Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar
es Salaam
24
Agosti, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
.gif)


0 Responses to “ RAIS MAGUFULI APOKEA TAARIFA YA UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA KUTOKA UGANDA HADI BANDARI YA TANGA”
Post a Comment