Thursday, September 15, 2016
DC MUFINDI AIFUNGIA SHULE YA SEKONDARI YA ST. JOSEPH ZADRASS KWA UTAPELI.
Do you like this story?
Mkuu wa wilaya aliyevalia koti la suti akizungumza na wanafunzi, waliojitambulisha kwamba wao ni kidato cha tatu. |
Mkuu wa wilaya na maofisa wa polisi na halmashauri wakikagua nyaraka shuleni hapo. |
Na fredy mgunda,Iringa
Mkuu wa wilaya ya Mufindi
Mh. Jamuhuri William ametoa muda wa siku 07 kwa mkuu wa shule ya sekondari ya
St. Joseph Zadrass iliyopo kata ya Rungemba katika kijiji cha Kitelewasi
Wilayani Mufindi, awe amerejesha fedha kwa wanafunzi takribani 70 aliowasajili
sanjari na kusitisha mpango wa utoaji elimu ya sekondari shuleni hapo baada ya
kubaini kuwa mmiliki wa shule hiyo anaendelea kudahili wanafunzi licha ya
kufutiwa usajili miaka nane iliyopita.
Taarifa ya liyotolewa na
kitengo cha habari na mawasiliano cha halmashauri ya Wilaya ya Mufindi,
imebainisha kuwa Mkuu wilaya ametoa maagizo hayo mara baada ya kufanya ziara ya
kushitukiza shuleni hapo na kuendesha zoezi la ukaguzi wa nyaraka za uhalali na
uhai wa shule hiyo.
Mh. William amesema, licha
ya shule hiyo kufutiwa usajili mnamo mwaka 2009 kwa kupoteza sifa, bado
imeendelea kusajili wanafunzi kwa mtindo wa kuwatapeli kwa ushirikiana na chuo
cha uwalimu cha Rungemba kwa hoja ya kuendesha masomo ya ziada kwa wanaotaka
kurudia mitihani wakati baadhi ya nyaraka zinaonesha hadi mwaka jana wamepokea
wanafunzi waliohamia kutoka shule nyingine ambazo zipo katika mfumo rasmi.
“Naagiza, ndani ya wiki
moja yaani ifikapo tarehe 20 mwezi huu wanafunzi wote wawe wameondoka,
nimemwagiza mkuu wa polisi wilaya na mdhibiti ubora wa elimu kusimamia zoezi
hilo na itakapofika tarehe 20 nitafuatilia utekelezaji wa agizo langu hili”
Aidha, Mkuu huyo wa wilaya
amewaonya wamiliki wote wa vyuo na shule Wilayani Mufindi Kuhakikisha wanaendesha
taasisi zilizosajiliwa na kuwataka wazazi na walezi kupeleka watoto
wao katika shule ambazo zinausajili wa serikali kwani mwisho wa siku watakuwa
wamepoteza fedha na Muda wa watoto wao na kusisitiza kuwa akiwa mkuu wa Wilaya
hiyo hatakubali kuona utapeli kama huo unatokea Wilani humo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “DC MUFINDI AIFUNGIA SHULE YA SEKONDARI YA ST. JOSEPH ZADRASS KWA UTAPELI.”
Post a Comment