Tuesday, September 27, 2016
KUIONA SIMBA VS YANGA KUANZIA 7,000. TICKET KUANZA KUUZWA KESHO.
Do you like this story?
SHIRIKISHO la mpira wa miguu Tanzania
TFF limetangaza viingilio vya mchezo wa 'Watani wa Jadi' Simba na Yanga wa ligi
kuu ya Vodacom Tanzania bara utakaofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam Jumamosi Octoba mosi.
Simba inakutana na watani wao wakiwa
vinara wa ligi baada ya kushinda Michezo mitano na kutoka sare mmoja huku Yanga
wakishinda minne, kutoka sare mmoja na kupoteza mmoja.
Afisa Habari wa TFF Alfred Lucas
amevitaja viingilio hivyo kuwa VIP A ni sh 30,000 VIP B & C sh 20,000 na
mzunguko utakuwa sh 7,000.
Mashabiki watakaotaka kushuhudia
mtanange huo uwanjani watatakiwa kutumia tiketi za Kielectoniki ambazo ndiyo
pekee zitakazowezesha kuutazama mchezo huo ambao unaziba mianya yote ya kuingia
bila kulipa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni
ya Selecom ambao ndiyo wasimamizi wa tiketi hizo Galus Runyeta alisema tiketi
hizo zitaanza kuuzwa kuanzia kesho katika vituo mbali mbali jijini hapa.
Baadhi ya vituo hivyo ni Vituo vya
mafuta vya Total, Village Supermarket, Vituo vya mafuta ya Puma, Samaki Samaki,
Buguruni Sheli, Mlimani City, Sinza Africa Sana na Uwanja wa Taifa.
Aidha Galus amewataka mashabiki wa
timu hizo kununua tiketi mapema kuanzia kesho katika vituo tajwa ili kuepuka
usumbufu utakaojitokeza siku ya mtanange huo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “KUIONA SIMBA VS YANGA KUANZIA 7,000. TICKET KUANZA KUUZWA KESHO.”
Post a Comment