Wednesday, September 28, 2016
SAMWELI SITTA APELEKWA UJERUMANI KUTIBIWA.
Do you like this story?
HALI
ya afya ya Spika mstaafu, Samuel Sitta si nzuri,baada ya Serikali kumpeleka
nchini Ujerumani kwa matibabu zaidi.
Habari
za uhakika zinasema Sitta alipelekwa Ujerumani juzi kwa matibabu baada ya
afya yake kubadilika ghafla.
“Nilimtembelea
siku moja kabla ya kupelekwa nje ya nchi, kwa kweli hali ya afya yake ilikuwa
imedhoofu, namwombea Mungu amsaidia apone haraka ili arudi kuendelea na
majukumu yake.
“Nimesikitishwa
mno na taarifa za kuzushiwa kifo mzee wangu huyu, Mungu ni mwema najua bado
anampigania uhai wake…hii tabia ya mitandao ya kijamii kumzushia mtu kifo sijui
inafaidika nini.
“Mpaka
anaondoka nchini kwenda matibabu natambua amekuwa asikumbuliwa mno na tatizo la
miguu, sasa mimi si daktari wake siwezi kuongeza zaidi,”kilisema chanzo chetu.
Septemba
19, mwaka huu, Rais Dk. John Magufuli alimtembelea Sitta hospitalini alikolazwa
kwa muda sasa kumjulia hali, kisha kumwombea dua Mungu amsaidie.
Siku
iliyofuata Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa naye alimtembelea hospitalini
kumjulia hali.
Sitta
ameshika nyadhifa mbalimbali, zikiwamo za Spika wa Bunge kuanzia mwaka
2005 hadi 2010, uwaziri na ubunge kwa kipindi kirefu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ SAMWELI SITTA APELEKWA UJERUMANI KUTIBIWA.”
Post a Comment