Thursday, September 15, 2016
TAARIFA KUHUSU MADEREVA WA TANZANIA KUTEKWA NA WAASI WA MAI MAI
Do you like this story?
Chama cha Wamiliki wa Magari ya Mizigo nchini Tanzania (TATOA)
kinaripoti kwamba, waasi wa Mai Mai nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
(DRC), wamewateka nyara madereva wa Tanzania na kuchoma baadhi ya magari ya
mizigo. Waasi hao wanadai dola za Kimarekani elfu nne (karibu shilingi za
Kitanzania milioni tisa) kwa kila dereva ama sivyo watawapiga risasi madereva
wote. Pia waasi hao wametoa siku ya mwisho (deadline) ya majeshi yanayolinda
amani nchini humo kuondoka.
TATOA inasema imezungumza na mmiliki wa kampuni ya Simba
Logistics, Mzee Azim Dewji ambaye amethibitisha taarifa hizi na pia balozi wa
Tanzania DRC pamoja na Wizara ya Mambo ya Nje tayari serikali inashughulikia
suala hili. Jumla ya magariyaliyotekwa ni 12 kati ya hayo magari 8 ya Tanzania
na 4 ya Kenya. Magari 4 ya Tanzania yamechomwa moto na madereva wote
walichukuliwa na waasi lakini bahati nzuri madereva wawili wa Tanzania
walifanikiwa kuwatoroka. Tukio hilo limetokea sehemu inaitwa Kasebebena na
Matete, wastani wa kilomita 30 kutoka mji wa Namoya.
TATOA inawashauri wanachama waliopakia mzigo kuelekea huko
kuwasiliana na madereva wao ili wasitishe safari, kusubiri taarifa ya hali ya
usalama kutolewa.
Mai Mai Kata ni kundi la waasi nchini DRC ambalo linadai kupigania
uhuru wa jimbo la Katanga, na linaongozwa na Gédéon Kyungu Mutanga, ambaye
aliunda kundi hilo mara tu alipotoroka kutoka gerezani mwaka 2011.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TAARIFA KUHUSU MADEREVA WA TANZANIA KUTEKWA NA WAASI WA MAI MAI”
Post a Comment