Tuesday, September 27, 2016
WATOTO 2,570 WARIPOTIWA KULAWITIA KWA KIPINDI CHA MIEZI SBA
Do you like this story?
Vitendo
vya ukatilitili wa kijinsia kwa watoto vimeendelea kuongezeka kwa kasi nchini
katika kipindi cha mwezi Januari hadi Julai mwaka huu ambapo zaidi ya watoto
2,570 wa kike na kiume wamelawitiwa na kubakwa.
Akizungumza
katika sherehe za maadhimisho ya miaka 21 ya Kituo cha Sheria na Haki za
Binadamu (LHRC) yaliyofanyika jana katika Makao makuu ya watoto yaliyopo
Kurasini jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC Helen Kijo-Bisimba
alisema idadi hiyo ni kubwa ukilinganisha na ya mwaka jana.
Hata
hivyo, Mama Bisimba alisema kwa mujibu wa Msemaji wa Jeshi la Polisi, takwimu
hizo zinaweza kuwa ndogo kutokana na kesi nyingi za ubakaji na ulawiti kwa
watoto kutoripotiwa polisi kwa sababu ya mila na desturi za maeneo mengi
nchini.
“Ripoti
ya Jeshi la Polisi kupitia dawati la jinsia kati ya Januari na Machi 2016
inaonyesha matukio ya watoto kubakwa na kulawitiwa yakiendelea kuongezeka
kutoka 180 hadi 1765 hayo ni matukio yaliyotolewa taarifa katika vituo
mbalimbali vya polisi nchi nzima ukilinganisha na matukio 1585 mwaka 2015. Hata
hivyo waliohusika na matukio hayo wameonekana wakirandaranda bila kuchukuliwa
hatua za kisheria, ” alisema.
Alisema
ripoti hiyo inaonyesha kuwa kesi 1,203 zipo katika hatua ya upelelezi, 822 zipo
mahakamani na watuhumiwa 234 wamekwisha hukumiwa.
“Pia
utafiti uliofanywa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto kwa
kushirikiana na Tanzania kitengo cha ustawi wa jamii unaonyesha kati ya watoto
10 wa kike 4 wamebakwa, na kati ya watoto 10 wa kiume 3 wamelawitiwa zaidi ya
mara tatu. Utafiti huo unaonyesha kwa ujumla kuwa watoto wa kike na wa kiume 6
walifanyiwa ukatili huo na watu ndani ya familia,” alisema.
Bisimba
alisema asilimia 49 ya ukatili hufanyika nyumbani, 23 hufanyika njiani wakati
wa kwenda shule au kurudi, na asilimia 15 hufanyika shuleni. Pia ripoti hiyo ya
UNICEF inaonyeaha kuwepo kwa matukio ya watoto kulawitiana na kubakana wenyewe
kwa wenyewe kutokana na kuvizoea vitendo hivyo.
LHRC
imeitaka serikali kupitia Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto pamoja na Wizara ya Katiba na Sheria kuifanyia marekebisho sheria ya
mtoto na kutilia mkazo malezi bora kwa watoto ikiwemo kuweka kipengele
kitakachotoa adhabu kali kwa familia itakayoshindwa kutoa malezi bora kwa
mtoto.
LHRC
inayoshughulika na utetezi wa sheria na haki za binadamu ilianzishwa Septemba
26, 1995.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ WATOTO 2,570 WARIPOTIWA KULAWITIA KWA KIPINDI CHA MIEZI SBA”
Post a Comment