Wednesday, October 5, 2016
JAJI MUTUNGI ATOA ONYO KALI KWA WANASIASA.
Do you like this story?
Kwa siku kadhaa sasa CUF imekumbwa na mgogoro wa
kiuongozi kati ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad na
Mwenyekiti wake aliyepata kujiuzulu na kurejea tena Profesa Ibrahim Lipumba.
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini ametoa onyo na
kuwataka wale wote wanaotumia vibaya jina la ofisi ya Msajili ili kuichafua
ofisi yake au kwa lengo la kukidhi hisia na matakwa yao binafsi waache kabisa
tabia hiyo,
“Tunauomba umma wa Watanzania kutambua kuwa Ofisi ya
Msajili wa Vyama vya Siasa ni taasisi inayoendeshwa kwa kufuata misingi na
taratibu za sheria za nchi. Aidha tunawaasa wadau wa habari kutoa taarifa baada
ya kujiridhisha na usahihi wa taarifa hizo, na kujikita kwenye taarifa zinatolewa
rasmi na Ofisi ya Msajili wa vyama vya Siasa badala ya kuuaminisha umma na
kuupotosha kwa makusudi,” ilieleza taarifa ya Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
ya Ofisi ya Msajili , Monica Laurent
Kwa upande wa Baraza la Udhamini la CUF kupitia kwa
Mwenyekiti wa kikao kilichoketi wiki hii na Mjumbe wa baraza hilo, Peter Malebo
alisema mgogoro uliopo ndani ya chama hicho utamalizwa ndani ya chama hicho
baada ya kuzikutanisha pande hizo mbili.
Aidha, Malebo alisema wanampongeza Msajili wa Vyama
vya Siasa, Jaji Francis Mutungi kwa kutolea ufafanuzi wa sakata la uongozi wa
chama hicho na kumthibitisha Profesa Lipumba kuwa ni Mwenyekiti halali wa chama
hicho kwa mujibu wa Katika ya chama chao
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “JAJI MUTUNGI ATOA ONYO KALI KWA WANASIASA.”
Post a Comment