Wednesday, October 19, 2016

KAKA YAKE BARACK OBAMA AKUBALI MWALIKO WA DONALD TRUMP





Kaka yake Rais wa Marekani Barack Obama, Malik Obama amekuwa shabiki mkubwa wa mgombea Urais nchini Marekani kupitia chama cha Republican Bw. Donald Trump, huku akiwahi kunukuliwa katika moja ya mahojiano yake na kituo kimoja cha redio nchini Kenya kuwa kaka Yake Baraka Obama hafai kuwa hata mfanyakazi wa duka.

Maafisa wa mgombea Trump wamethibitisha wamethibitisha kumwalika Malik katika moja ya midahalo ambapo atakuwa miongozi mwa hadhira itakayofuatilia mdahalo huo wa runinga, Bw Trump akikabiliana na mpinzani wake wa chama cha Democratic Hillary Clinton.

Malik, aliambia gazeti la New York Post kwamba ana furaha isiyo na kifani kwamba atahudhuria mdahalo huo.
"Trump anaweza kuirejeshea Marekani fahari yake tena," amesema, kwa mujibu wa shirika la habari la AP.

Wagombea wamekuwa wakitumia wageni kwenye midahalo kama njia ya kuwakabili wapinzani wao.

Bi Clinton amekuwa akiwaalika wakosoaji wakuu wa Bw Trump, bilionea Mark Cuban na afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya Hewlett Packard Enterprise Meg Whitman.

Katika mdahalo wa pili, Bw Trump alialika wanawake watatu amabao walimtuhumu rais wa zamani Bill Clinton kwa kuwadhalilisha kingono miaka ya nyuma.

Malik Obama amekuwa akikosoa utawala wa kakake Rais Barack Obama

0 Responses to “KAKA YAKE BARACK OBAMA AKUBALI MWALIKO WA DONALD TRUMP”

Post a Comment

More to Read