Monday, October 24, 2016

LWANDAMINA KOCHA MPYA YANGA



Zikiwa zimepita wiki mbili tangu Katibu Mkuu wa Yanga Baraka Deusdedit akanushe taarifa za klabu ya Yanga kutaka kumfukuza kocha wake Hans Van Pluijim na kumpatia mikoba kocha kutoka Zambia George Lwandamina, leo kocha huyo amewasili katika kiwanja cha kimataifa cha ndege cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam na kuthibitisha uvumi huo.
 



Taarifa kutoka chanzo chetu cha Habari zinasema kuwa kocha huyo kutoka Taifa la Zambia ameingia mkataba wa kuifundisha klabu ya Yanga kwa muda wa Miaka 2 huku Mwenyekiti wa Yanga SC, Yusuf Manji na Hans van der Pluijm wakiingia makubaliano ya kumbakisha Pluijim kama kama Mkurugenzi wa Ufundi (Technical Director) kwa klabu ya Yanga.


Taarifa zinaenda mbali na kusema kuwa baada ya ligi kusimama kocha George Lwandamina ataenda kuweka kambi nje ya nchi huku uongozi wa klabu ya Yanga ukiweka mipango kwa nchi ya Brazil au Ureno.

 


0 Responses to “LWANDAMINA KOCHA MPYA YANGA ”

Post a Comment

More to Read