Wednesday, February 22, 2017
DKT,ABBAS AWATAKA MAOFISA HABARI KUYAZUNGUMZIA MAZURI YA SERIKALI
Do you like this story?
Hayo yalisemwa wakati wa uzinduzi wa tovuti za halmashauri 35 za mikoa mitano ya kanda ya Ziwa inayojuimuisha Mikoa ya Mwanza,, Kagera, Mara, Shinyanga, na Simiyu.
Dkt.Abbas alisema pamoja kuwepo kwa vyombo mbalimbali vya habari vinavyotumika kufikisha taarifa za habari kwa wananchi ikiwemo magazeti na redio, bado mitandao ya kijamii ikiwemo barua pepe imeendelea kutumiwa na wananchi wengi zaidi ulimwenguni kwa sasa.
”Kwa sasa nusu ya watu duniani wapo mtandaoni na hapa nchini kwa mujibu wa ripoti ya TCRA (Mamlaka ya Mawasiliano Nchini) inaonesha kuwa watanzania zaidi ya milioni 19 wapo mtandaoniaidha kwa kutumia barua pepe, au kutembelea kurasa facebook,” amesema Dkt.Abbas.
Dkt. Abbas ameeleza sifa za Ofisa Habari na Mawasiliano wa karne ya sasa ni mwenye uwezo wa kutumia njia za kisasa za mawasiliano, ambazo zitamwezesha kujibu hoja mbalimbali kwa haraka zaidi, badala ya kusubiri serikali kulalamikiwa na wananchi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “DKT,ABBAS AWATAKA MAOFISA HABARI KUYAZUNGUMZIA MAZURI YA SERIKALI”
Post a Comment