Wednesday, February 22, 2017

JUMA KASEJA ASHINDA TUZO YA MCHEZAJI BORA





Mlinda mlango wa Klabu ya Kagera Sugar Juma Kaseja ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu Vodacom Tanzania bara kwa mwezi Januari akimtupa nje Jamal Mtegeta Golikipa wa Klabu ya Toto African.

 
Vodacom ambao ndiyo wadhamini wa Ligi kuu wamemtangaza Juma Kaseja kuwa ndiyo mchezaji bora kwa mwezi Januari kwa kuandika “Kipa wa KageraSugar, Juma Kaseja amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom wa mwezi Januari kwa msimu wa 2016/2017
Kaseja amecheza michezo mitatu na kuruhusu goli moja tu huku akiisaidia timu yake kushinda michezo mitatu na kufunga magoli 6 kwa mwezi Januari,Anakuwa ni Goli kipa wa kwanza kupokea Tuzo hiyo toka zianzishwe ambapo mchezaji bora wa mwezi huzawadiwa Fedha Taslim Tsh Milioni 1.

0 Responses to “JUMA KASEJA ASHINDA TUZO YA MCHEZAJI BORA ”

Post a Comment

More to Read