Wednesday, February 22, 2017

MCHUNGAJI AAMBULIA KICHAPO KANISANI


Waumini wa kanisa la Anglikana la Mtakatifu Yohana, Dayosisi ya Victoria Nyanza, Parishi ya Bomani wilayani Sengerema, mkoai Mwanza wamemshushia kipigo  Mchungaji wa kanisa hilo, Joseph Kwangu wakati wa ibada ya jumapili ikiendelea, baada ya waumini hao kumtuhumu mchungaji kufanya mambo yanayoendana na ishara wanazozitumia Freemason.
Waumini hao waliamua kubandika matangazo ndani ya kanisa, vyooni, milango ya kuingilia kanisani kumtaka mchungaji huyo asiingie ndani ya kanisa hilo.
Mchungaji huyo alikaidi maagizo ya waamini hao na kutaka kuingia kanisani kinguvu jambo lililosababisha waamini hao kumtoa kwa nguvu na kumshushia kipigo na kusababisha vurugu kubwa.
Mara baada ya mchungaji huyo kushushiwa kipigo aliamua kukimbia na mke wake, ili kunusuru maisha yao, lakini vurugu hizo ziliendelea kwa dakika 30, hadi jeshi la polisi lilipowasili na kuwatuliza waumini hao.
Katibu wa kanisa hilo Mussa Mwebesa alisema: ” Huyu mchungaji baada kutoka Tanga kwenye mafunzo, alirudi akiwa amevaa kofia nyeusi pamoja na pete, Kanisa lilikuwa halina imani naye. Wakati wa kuendesha ibada huwa anatoa ishara za kukunja vidole. Tulikaa na vikao kumuuliza kuhusu mambo hayo alikosa majibu”.
Katibu huyo alisema walitoa taarifa kwa Askofu wa kanisa hilo abadilishwe kanisa laikni mchungaji huyo hata aliposhauriwa na waamini kuacha matendo hayo, alikana kufanaya hivyo jambo ambalo liliwakwaza wauminiwa kanisa hilo.

0 Responses to “MCHUNGAJI AAMBULIA KICHAPO KANISANI”

Post a Comment

More to Read