Thursday, February 23, 2017

ISRAELI ILIALIKA WASHINDI 26 WA TUZO ZA OSCAR,MPAKA SASA HAKUNA ALIYEKWENDA


56d34c31c361887b278b4606
Mwaka mmoja uliopita, serikali ya Israel ilialika mastaa wa filamu Leonardo DiCaprio, Matt Damon na waigizaji wengine maarufu wakiwalipia kila kitu kwa safari za kifahari, lakini mpaka sasa hawajaitikia mualiko huo.
Wapigadomo wanashangilia kitendo hicho kuwa ni kama ushindi kwakuwa hakuna hata mmoja aliyekubali mualiko huo kati ya mastaa hao 26 ambao walikuwa washindi wa tuzo za filamu za Oscar katika miaka mbalimbali. Ilitegemewa kila mmoja katika mastaa hawa atatumia kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 123.
Kwenye ofa hiyo, walikuwa pia wapewe vifurushi vya zawadi kutoka kwa kampuni moja ya matangazo, ilikuwa kila mmoja apewe kifurushi cha zawadi kinachokadiriwa kufikia shilingi milioni 447.
Idadi ya wanachama wa Chama cha Democrats nchini Marekani ambao wanaonekana kuwaunga mkono zaidi Wapalestina kuliko Waisrael imekuwa ikiongezeka kwa zaidi ya mara mbili sasa ikilinganishwa na ilivyokuwa mwaka 2014, hii ni kwa mujibu wa matokeo ya utafiti uliofanywa na Taasisi ya Tafiti ya Pew.
Makundi yanayoendesha kampeni mbalimbali za kijamii yanailaumu Israel kwa kutaka kuwatumia watu maarufu ili kupata sifa nzuri kwenye vyombo vya habari vya kimataifa na kuzima habari dhidi yake kuhusu ukatili inaoufanya kwenye makazi ya raia wa Palestina.
Zikiwa zimesalia siku chache kabla ya sherehe za kutoa tuzo za Oscar kwa mwaka 2017 ambazo zitafanyika Februari 26, hakuna mualikwa hata mmoja ambaye amehudhuria yeye binafsi.
Staa wa filamu ya Hunger Games, mwanadada Jennifer Lawrence alikubali mualiko huo lakini akawapa wazazi wake akisema kuwa wakala wake wamepata filamu mpya anayotakiwa kuigiza hivi karibuni, kwahiyo hatoweza kusafiri.
“Haya ni mafanikio kwetu,” alisema Yousef Munayyer kutoka taasisi ya Kimarekani Inayotetea Haki za Wapalestina, ambayo iliendesha kampeni dhidi ya safari hizo pamoja na Taasisi nyengine ya Kimarekani iitwayo Sauti ya Wayahudi kwa ajili ya Amani.
“Nashukuru kwamba hakuna aliyeenda. Nadhani ni wazi sasa inaonekana kuwa kuwaalika wacheza filamu ilikuwa mbinu ya kuhamisha mawazo ya watu, lakini imeshindikana.”
Waziri wa Utalii wa Israel ameshindwa kukataa au kutoa namba ya idadi ya waigizaji walifika kama wapo hata wachache waliofika.
Mambo yawabadilikia Israeli
Msemaji wa Sauti ya Wayahudi kwa ajili ya Amani, Bi. Granate Sosnoff alisema kuwa hii ni miongoni tu mwa mgomo mkubwa wa jamii mbalimbali dhidi ya uonevu huu wa Israeli.
“Kampeni zetu zimeongeza taharuki, zimeingilia kati jina lilikuwa linaonekana tukufu la Israel na zimeikumbusha mastaa wa Hollywood kwamba kuna gharama kubwa za kijamii zilizosababishwa na uvamizi wa kijeshi uliofanywa na Israeli katika makazi ya Wapalestina,” alisema.
Dan Rothem, mtafiti kuhusu uhusiano baina ya Marekani na Israel, alisema kuwa Israel ilitaka kuwatumia watu maarufu “kama njia yao ya kuondoa muonekano wa sasa wa kuwepo kwa mgomo au kutengwa na nchi nyengne”.
Wanamuziki wanaofanya matamasha nchini Israeli wanapata msukumo mkubwa kutoka kwa wanaharakati wakiwataka wanamuziki hao wagome pia, ambapo mwanamuziki Pink Floyd’s Roger Waters akiwa kiongozi mkuu wa kampeni hizi.
Wiki iliyopita, utata uliibuka baada ya timu ya Mpira wa Kimarekani kutakiwa kutembelea Israel ambapo wachezaji watano tu kati ya 11 za ligi kuu ya NFL baada ya fainali ya Superbowl.
Mchezaji wa ulinzi wa timu ya Seattle Seahawks, Michael Bennett alisema kuwa “hatakubali kutumika kwenye propaganda” za Israel.
“Nikienda Israeli — na nitakwenda — itakuwa ni kwa ajili ya kuona sio tu Israeli bali atakwenda pia kuona maeneo ya Ukingo wa Gaza ili nione na Wapalestina, ambao wamekuwa kwenye ardhi hiyo kwa maelfu ya miaka wakiishi maisha yao,” mchezaji huyo alisema.
“Watu wa mrengo wa kusho na mrengo wa kulia waliopo nchini Marekani kwa sasa hawaingalii Israel kwa namna ile ile waliyokuwa wakiiona mwano,” alisema Rothem.

0 Responses to “ISRAELI ILIALIKA WASHINDI 26 WA TUZO ZA OSCAR,MPAKA SASA HAKUNA ALIYEKWENDA”

Post a Comment

More to Read