Thursday, February 23, 2017
PICHA;MAASKOFU WAUNGANA KUMUOMBEA RAIS DKT MAGUFULI
Do you like this story?
Askofu wa Kanisa la Good News for All
Ministry Dkt. Charles Gadi kwa niaba ya Viongozi wa Dini na Madhehebu
mbalimbali hapa nchini wamempongeza Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa
kumteua Kamishna wa Mamlaka ya Kuthibiti na Kupambana na Dawa za
Kulevya.
Dkt. Gadi ametoa pongezi hizo leo,
Jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea na vyombo vya habari katika
ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO).
“Tunamshukuru Mungu kwa kumuinua Rais
ambaye ameonyesha nia na kuwa mstari wa mbele kupigana na biashara hiyo
haramu, ni ukweli usiopingika kwamba tatizo la dawa ya kulevya ni
kubwa na lenye madhara makubwa sana kwa watanzania wengi haswa vijana
ambao ni nguvu kazi ya Taifa,” alifafanua Dkt. Gadi.
Aliendelea kwa kusema kuwa, Vijana wengi
wamepoteza maisha, kuharibika akili, kupata magonjwa ya kuambukiza,
kupoteza malengo ya kimaisha kwa sababu ya dawa hizo. Vile vile dawa
hizo zimeleta fedheha kwa Taifa kutokana na Vijana wengi wa Kitanzania
kuwepo katika magereza mbalimbali Duniani huku wengine wakisubiri
adhabu ya kunyongwa.
Aidha amempongeza Rais Dkt. Magufuli kwa
kuimarisha Mamlaka ya Kuthibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa
kumteua Kamishna ambaye atasimamia Mamlaka hiyo na anaamini kwamba kwa
neema ya Mungu ataweza kumsaidia kikamilifu Rais Magufuli katika
kutimiza azma yake ya kukomesha biashara hiyo.
Wakati huo huo, Dkt. Gadi amempongeza
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kwa kuianzisha vita hiyo
dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya katika mkoa wa Dar es Salaam. Vile
vile amewapongeza waandishi wa habari na vyombo mbalimbali vya habari
kwa kutoa habari zinazosaidia katika upambanaji wa biashara hiyo.
Dkt. Gadi amewataka viongozi wa Dini
kuungana bega kwa bega na Rais Magufuli kwa kuendelea kutoa maadili kwa
vijana ili kuepukana na uovu wa dawa za kulevya nchini.
Askofu
wa Kanisa la Good News for All Ministry Dkt. Charles Gadi (wa tatu
kutoka kushoto) pamoja na Maaskofu wa Madhehebu Mbalimbali wakimuombea
Rais Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya mkutano na waandishi wa
habari (hawapo pichani) katika ukumbi wa Idara ya Habari -MAELEZO, leo
Jijini Dar es Salaam.
Maaskofu
wa Madhehebu mbalimbali wakimuombea Rais Dkt. John Pombe Magufuli mara
baada ya mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika ukumbi
wa Idara ya Habari -MAELEZO,leo Jijini Dar es Salaam.
Maaskofu
wa Madhehebu mbalimbali nchini wakiongozwa na Askofu wa Good News for
All Ministry Dkt. Charles Gadi (wa tatu kutoka kushoto) wakiombea
Bendera ya Tanzania ili Amani iendelee kutawala nchini.
Maaskofu
mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mkutano na
vyombo vya habari uliolenga kumuombea na kumpongeza Rais Magufuli kwa
kumteua Kamishna wa Kupambana na Kuthibiti Matumizi ya Dawa za kulevya
nchini.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “PICHA;MAASKOFU WAUNGANA KUMUOMBEA RAIS DKT MAGUFULI”
Post a Comment