Friday, February 24, 2017
KIMBUNGA DORIS CHAUA
Do you like this story?
Mwanamke mmoja
amepoteza maisha na watu wengine wawili wamejeruhiwa vibaya, baada ya
kimbunga Doris kupiga mji wa Wolverhampton nchini Uingereza kwa kasi ya
kilomita 94 kwa saa.
Imeelezwa kuwa mwanamke huyo alipata majeraha kichwani baada ya vipande vya mabaki ya vitu kuanguka katika mtaa mjini humo.
Upepo huo mkali umesababisha safari za ndege kusitishwa huku pia huduma za usafiri wa barabara na reli kusimamishwa.
Maelfu
ya makazi na biashara zipatazo 1,500 kaskazini mwa Ireland zimeachwa
bila ya huduma za umeme, huku milingoti na nyaya ya umeme zikiangukiwa
na miti.
Taarifa kutoka kwa shirika la kawi nchini Uingereza imesema kuwa, karibu watu 12, 030 hawana nguvu ya umeme.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “KIMBUNGA DORIS CHAUA”
Post a Comment