Wednesday, March 1, 2017
DC NJOMBE AMTANDIKA MAKOFI MWENYEKITI WA MTAA.
Do you like this story?
Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi Ruth Msafiri Amejikuta akimtandika makofi Mwenyekiti wa Mtaa wa Buguruni –Matalawe Emmanuel Ngelime mara baada ya kutokuwepo kwa maelewano baina ya viongozi hao wawili.
Mapema katika ziara ya kushtukiza ya mkuu huyo wa wilaya katika ofisi ya
mtaa wa Buguruni Mjini Njombe kumeibuka hali ya Taharuki iliyomfanya mkuu wa wilaya kushindwa kuzuia hasira zake na kumtandika makofi mwenyekiti huyo.
Imebainika
kuwa Mpaka sasa Mwenyekiti wa Mtaa huo Bwana Emmanuel Ngelime
Anatumikia kifungo cha Nje cha Mwaka Mmoja kwa kosa la kujaribu kumbaka
mwanamke mmoja mtaani kwake.
Mara
Kadhaa Mkuu huyo wa wilaya amesikika akimtaka Mwenyekiti huyo
kutojihusisha na maswala ya kazi kama kiongozi wa mtaa lakini Mwenyekiti
Huyo amekuwa akikaidi kwa kuendelea kufanya kazi ili hali amekosa sifa
ya kuwa Mwenyekiti.
Ziara ya mkuu wa wilaya imefuatia mara baada ya kupewa taarifa za kuwa mwenyekiti
wa serikali ya mtaa huo amehukumiwa kwa kifungo cha mwaka mmoja kwa
madai ya kutaka kumwingilia kingono mwanamke mmoja mtaani hapo bila
ridhaa yake .
Hata
hivyo tafsiri ya sheria imeweka wazi kuwa kiongozi yeyote wa serikali
atakae hukumiwa kifungo cha zaidi ya miezi sita basi kisheria atakuwa
amepoteza uharali wa kuwa kiongozi katika nafasi yoyote kwa mujibu wa sheria.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 Responses to “DC NJOMBE AMTANDIKA MAKOFI MWENYEKITI WA MTAA. ”
March 2, 2017 at 8:29 AM
Hatari kweli
Post a Comment