Wednesday, March 1, 2017

MBATIA ATOA NENO


Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia amewashukuru watu mbalimbali ambao wamekuwa wakimfariji wakati akiendelea na matibabu ya mguu unaomsumbua.
Akizungumza jana nyumbani kwake Mbezi Beach jijini hapa, Mbatia alisema kumekuwa na minong’ono kuwa anaumwa ugonjwa ambao hautibiki.
Hata hivyo, alisema anaendelea vizuri na kwamba wakati wowote anaweza kuanza kuendelea na majukumu yake kama kawaida.
“Mtu akifa watu wanalia na kulalamika lakini baada ya kuzika kila mtu ananawa mikono na ataelekea anakokujua, lakini rafiki wa kweli anafahamika wakati wa shida hapo ndiyo unajua kwamba hata siku usipokuwa dunia watoto, mke na ndugu hao ndiyo watawajulia hali,” alisema Mbatia.

0 Responses to “MBATIA ATOA NENO”

Post a Comment

More to Read