Wednesday, March 1, 2017
TAADHARI TOKA MAMLAKA YA HALI YA HEWA NCHINI
Do you like this story?
Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA) imewashauri wananchi na Mamlaka
za Miji kuhakikisha kuwa mifumo na njia za kupitisha maji katika maeneo
yao inafanya kazi kwa kiwango cha kutosha ili kuepuka madhara
yanayoweza kutokana na mvua za msimu zinazotarajiwa kuanza mwezi Machi.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini
(TMA) Dkt. Agnes Kijazi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari
Jijini Dar es salaam kuhusu mwelekeo wa msimu wa mvua Tanzania katika
kipindi cha mvua za masika kuanzia Machi hadi Mei.
Amesema kuwa yapo maeneo ambayo yatapata mvua za wastani na juu ya
wastani na wengine chini ya wastani hivyo ni vema wananchi wakachukua
tahadhari ili kuepuka madhara mbalimbali ambayo yanaweza kuwapata
kutokana na mvua hizo.
Dkt. Kijazi ameongeza kuwa mvua hizo zinaweza kusababisha maji
kutwama katika baadhi ya maeneo ya hivyo kusababisha mafuriko ambayo
yatapelekea kuzuka kwa magonjwa ya mlipuko na uharibifu wa miundombinu
mbalimbali ikiwemo mifumo ya maji na barabara.
Aidha ,Mkurugenzi Mkuu amesema kuwa hali ya unyevunyevu katika udongo
inatarajiwa kuimarika kiasi cha uzalishaji wa malisho ya mifugo na
ukuaji wa mazao katika baadhi ya maeneo kuongezeka .
Hata hivyo , Mkurugenzi Mkuu huyo amewashauri wafugaji kuwa na mifugo
ambayo inalingana na uwezo wa malisho yaliyopo kulingana na ushauri wa
Maafisa Mifugo.
Dkt. Kijazi ameyataja maeneo ambayo yanatarajiwa kuwa na mvua ya
wastani na juu ya wastani kuwa ni Dodoma, Singida, Kigoma, Tabora,
Rukwa, Katavi, Mbeya na Iringa.
Maeneo ambayo yanatarajiwa kupata mvua za juu ya wastani ni njombe, Ruvuma, Lindi, Mtwara, na kusini mwa Morogoro.
Amesema kuwa ukanda wa Ziwa Victoria na maeneo ya Pwani ya Kaskazini
mvua zinazoendelea kunyesha zinatarajiwa kuungana na msimu wa Machi na
kusambaa katika maeneo mengine.
Dkt. Kijazi amesema kuwa maeneo ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro ,
Tanga, Dar es Salaam, Kaskazini mwa Morogoro na Visiwa vya Unguja na
Pemba yanatarajiwa kuwa na mvua za chini ya wastani na vipindi virefu
vya ukavu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ TAADHARI TOKA MAMLAKA YA HALI YA HEWA NCHINI”
Post a Comment