Monday, March 27, 2017
MFAHAMU MWANAMITINDO ANAYEUGUA UGONJWA WA PAKA
Do you like this story?
Mwanamitindo
wa Uingereza, Caitin Stickels mwenye umri wa miaka 29, amekuwa
akisumbuliwa na tatizo ambalo ni nadra sana la kiafya linalofahamika
kama ‘Ugonjwa wa macho ya paka’ unaojulikana kitaalamu kama
‘Schmid-Fraccaro Syndrome.’ ambao humsababishia maumivu makali sana.
Tatizo hilo la kiafya humfanya aonekane kama paka.
Hali yake ilimvutia mpiga picha za mitindo kutoka Uingereza Nick
Knight. Alimuona mwanamitindo huyo kutoka Seattle mara ya kwanza kwenye
ukurasa wake wa Instagram.
Hata hivyo mwanamitindo huyo bado anafurahishwa na mafanikio aliyoyapata licha ya kusumbuliwa na ugonjwa huo.
“Ni mabadiliko makubwa zaidi mema yaliyowahi kutokea katika maisha yangu,” alisema.
Watu wanaougua ugonjwa huo wanaweza kuwa na matatizo katika maumbile
ya masikio yao, moyo na kwenye figo. Wakati mwingine, viungo vingine
mwilini huathiriwa.
Sura ya Caitin si kama ya wanamitindo wengi ambao wamevuma sana.
‘Urembo’ wake si kama ule ambao wengi wamezoea kuuona ukiangaziwa kwenye
majarida, filamu na runinga.
Alisema “Sikuwahi kuwa na ndoto ya kuwa mwanamitindo au kufikiria ningeshiriki katika tasnia ya mitindo na mavazi,”
Aliongeza kuwa huwa anakumbana na changamoto kadhaa katika maisha yake kutokana na ugonjwa huo unaomsumbua.
“Mafadhaiko kutokana na ugonjwa huu huwa ni ndani ya moyo
wangu, lakini kazi yangu ya uanamitindo, uigizaji na uimbaji hunisaidia
sana kusahau maumivu niliyo nayo moyoni.” anasema.
Caitin anasema pia hupata maumivu makali mwilini na kupata kichefuchefu.
“Ni figo moja pekee inayofanya kazi, kwa hivyo huwa
inanibidi kunywa maji sana. Pia mwili wangu huathiriwa sana na
mabadiliko katika mazingira, lakini kwa sababu umekuwa hivyo kwa muda
mrefu, watu wengi niliotangamana nao huwa hawatambui kama nina tatizo.
Mimi ni mgumu kama jiwe.”
“Nafikiri jambo jingine ni kwamba macho hukaa kama ya
paka wakati wote na kusababisha watu kuniogopa. Hii hata hivyo
huniwezesha kuona vyema usiku. Nalipenda jua na mara nyingi hutoka nje
na kutembea, lakini huwa linaniumiza macho yangu.”
Vile vile aliongeza kuwa pamoja na hali yake, baadhi ya watu
wamemzoea na humchukulia kama mtu wa kawaida tu japo kwa nyakati zingine
baadhi yao humuogopa hasa watoto wanapokutana naye kwa mara ya kwanza.
Alisema kuwa anafurahishwa na jamii inayomzunguka kwa kuwa humtunza kama mmoja wao na haimtengi.
“Watoto wakati mwingine ndio hunishangaa. Lakini mara nyingi huwa sikabiliwi na unyanyapaa.
Aidha alizungumzia kuhusu maisha yake ya utotoni na kusema kuwa
pamoja na yote aliyokumbana nayo, huwa anayakubali kwa kuwa hakuna
binadamu aliye mkamilifu chini ya mbingu.
“Utoto wangu ulikuwa vile vile. Watoto ni watoto tu, ni
kweli walinicheka na kunichezea. Lakini nani hakufanyiwa hivyo?, sote
huwa na kasoro pahala fulani. Hakuna aliyekamilika,”
Hizi ni baadhi ya picha za mwanamitindo huyo akiwa katika mionekano tofauti.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MFAHAMU MWANAMITINDO ANAYEUGUA UGONJWA WA PAKA”
Post a Comment