Friday, March 24, 2017
MWANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI ASIMULIA ALIVYOFANYA MAPENZI NA WALIMU WATATU
Do you like this story?
Mwanafunzi
wa Shule ya Msingi Ruwenzera amedai kufanya ngono na walimu wake watatu
kwa nyakati tofauti baada ya kuahidiwa kupewa zawadi na fedha.
Akizungumzia
sakaa hilo, mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo, Masele Omary alisema
kuwa Machi 7 uongozi ulikutana na kufikia uamuzi wa kumuomba mkurugenzi
mtendaji wa wilaya awaondoe walimu hao baada ya kujiridhisha na maelezo
yaliyotolewa na mwanafunzi huyo.
Kwa
mujibu wa mwanafunzi huyo anayesoma darasa la saba, alifanya ngono na
walimu hao kwa nyakati tofauti baada ya kumshawishi kumpa Sh10,000 na
mwingine kuahidi kumnunulia nguo za ndani.
Alidai
mwalimu Gerard Paulo alimuahidi kumnunulia nguo za ndani, huku Osner
Yohana na mwingine (jina linahifadhiwa kwa kuwa hakupatikana kuzungumza)
alimshawishi kwa kumpa Sh10,000 kila mmoja.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti, Paulo na Yohana walikana kumrubuni mwanafunzi huyo
wakidai tuhuma hizo zinatokana na wao kuhoji matumizi ya fedha za
ukarabati na michango ya chakula.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)