Tuesday, March 28, 2017

PICHA ZA KUCHEKESHA NA REKODI KUMI (10) ZILIZOVUNJWA BAADA YA 7-1 BRAZIL VS GERMANY (Branyukwaaaa!)


1.Kipigo Kikubwa zaidi katika historia ya brazil mara ya mwisho walifungwa 6-0 na Uruguay mwaka 1920 (miaka 94 iliyopita)
2. Ushindi mkubwa zaidi kwenye Mechi ya Nusu Fainali ikiishinda rekodi ya argentina ya 6-1 mbele ya USA
3. Brazil ilikuwa haijawahi kufungwa nyumbani toka mwaka 1975 walipopigwa 3-1 na Peru
4.Miloslov Klose awa mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi katika historia ya kombe la dunia baada ya kufikisha mabao 16
5. Kwa mara ya kwanza yanafungwa magoli Manne ndani ya Dakika sita
6. Mpaka mechi hiyo inamalizika, Brazil ilikuwa imeshafungwa mabao 11 kwenye michuano ya mwaka 2014 ikilingana na mwaka 1938 walipofungwa mabao 11 mpaka michuano inamalizika
7.Tukio la Soka lililosambaa zaidi kwenye mitandao ya kijamii katika historia ya kombe hilo
8 Kwa mara ya kwanza mwenyeji anafungwa goli 7 tangu kombe hilo lianzishwe
9. Mtu mmoja kufunga Goli Mbili ndani ya Sekunde 70!

10. Wajerumani waandika rekodi,  wafika Fainali kwa mara ya nane. Brazil ni wa pili, wamefika fainali ya kombe la dunia mara  7.


0 Responses to “PICHA ZA KUCHEKESHA NA REKODI KUMI (10) ZILIZOVUNJWA BAADA YA 7-1 BRAZIL VS GERMANY (Branyukwaaaa!) ”

Post a Comment

More to Read