Tuesday, March 28, 2017
MASHABIKI WA KIAFRIKA WAVAMIA UWANJA
Do you like this story?
Mchezo wa kimataifa wa kirafiki kati ya Senegal dhidi ya Ivory
Coast uliochezwa jijini Paris nchini Ufaransa, ulilazimika kusitishwa
kabla ya dakika 90, baada ya mashabiki kuvamia sehemu ya kuchezea dakika
ya 88.
Tukio hilo lilitokea ikiwa tayari timu hizo za Afrika magharibi zikiwa zimefungana bao moja kwa `moja.
Mwamuzi Tony Chapron aliwaamuru wachezaji kurejea katika vyumba vya
kubadilishia, kwa kuhofia hali ya usalama wao ambayo huenda ingeharibiwa
na mashabiki waliovamia sehemu ya kuchezea.
Wahusika wa usalama walijitahidi kuwaondoa mashabiki sehemu ya
kuchezea, lakini hatua hiyo ilishindikana na kumlazimu mwamui kumaliza
mchezo huo.
Mshambuliaji wa Liverpool Sadio Mane alikua wa kwanza kuipatia
Senegal bao la kuongoza kwa mkwaju wa penati dakika ya 68, lakini Gohi
Cyriac aliisawazishia Ivory Coast dakika tatu baadae.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MASHABIKI WA KIAFRIKA WAVAMIA UWANJA”
Post a Comment