Wednesday, March 29, 2017
MUME AMKIMBIA MKEWE BAADA YA MTOTO WAO KUPATA ULEMAVU
Do you like this story?
Mama
Amina Mkadingile mkazi wa kijiji cha Likonde wilaya ya Mtwara vijijini
ameomba watanzania kumsaidia matibabu ya mtoto wake Mwanaidi Hamisi wa
darasa la tano aliyepata ulemavu wa mikono baada ya kuungua moto akiwa
shuleni,tukio lililopolekea mume wake kumkimbia kukwepa majukumu ya
kuuguza mtoto huyo.
Akiongoea
kwa uchungu mama Amina Mkadengile anasema mtoto wake mwanaidi alipata
ulemavu huo akiwa shuleni baada ya kusukumwa na mwenzake kwenye shimo la
kuchomea taka katika shule ya msingi likonde na hivyo kuungua vibaya
mikono yake miwili, na hivyo kusaidiwa matibabu ya mkono mmoja na Ofisi
ya elimu mkoa wa Mtwara, huku mkono wa pili ukiwa bado unaitaji
matibabu.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Likonde amekiri mama Mkandengile
kuhangaikia matibabu ya mtoto wake pekee,hali iliyolazimu chama cha
msaada wa kisheria kwa wanawake na watoto mkoani Mtwara Paraligo
kumsaidia mama huyo kupata haki zake.
Matibabu
ya mkono wa pili yanahitaji gharama ya shilingi milioni moja huku
akitoa namba zake za simu kwa mtu atakayewiwa kumsaidia ambazo ni
0787894070
Subscribe to:
Post Comments (Atom)