Wednesday, March 29, 2017
KAMATI TA ULINZI NA USALAMA YA WILAYA IRINGA YAVAMIA BWAWA LA MTERA
Do you like this story?
Halmashauri
ya wilaya ya Iringa kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama ya
wilaya hiyo wamefanya msako wa kukamata nyavu aina ya Makokoro
zinazotumika kuvua samaki wadogo wasioruhusiwa kuvuliwa katika bwawa la
Mtera mkoani Iringa na kufanikiwa kukamata zana haramu za uvuvi 60
watuhumiwa 12 na kilo za samaki wadogo wakavu na wabichi 1227.
Msako
huo ulioanza majira ya saa kumi alfajiri umewajumuisha jeshi la polisi
wakiongozwa na mkuu wa polisi wilaya ya Iringa pamoja na ofisi ya
mshauri wa mgambo wilaya umelenga kukamata samaki wadogo wanaovuliwa
kinyume cha sheria katika bwawa hilo kama anavyofafanua kiongozi wa
operesheni hiyo Joseph Chitinka ambaye ni mwakilishi wa mkuu wa wilaya
ya Iringa.
Kaimu
mkurugenzi wa halmashauri ya Iringa Bibi Lucy Nyalu anasema operesheni
hii ni endelevu kwa lengo la kukomesha matumizi ya zana zisizostahili
katika shughuli ya uvuvi katika eneo lake huku afisa uvuvi kata ya
migori baraka uchimbira akiwataka wavuvi hao kukata leseni ili kufanya
shughuli hiyo kihalali na kuepuka usumbufu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)