Friday, March 31, 2017

SIKILIZA SAUTI: MAKONDA ALIKIMBIA SWALI LA VYETI ALILOULIZWA NA MWANAFUNZI


Dar es Salaam, Tanzania - 2015-08-29  -  The Most Muscular Man Tanzania competition in Dar es Salaam, Tanzania on August 29, 2015.  Photo by Daniel Hayduk
Mkuu wa Mkoa Dar es Salaa, Paul Makonda akiwa mkoani Dodoma alizua gumzo baada ya kuulizwa swali na mwanafunzi mmoja kuhusu tuhuma za vyeti vyake zinazomkabili ambapo kwa siku zote amekuwa yupo kimya kuhusu tuhuma hizo.
Mwanafunzi huyo alimuomba RC Makonda kulitolea ufafanuzi tuhuma za vyeti inayomkaili kama suala hilo lipo ndani ya uwezo wake kwani ni kiu ya watu wengi kutaka kuufahamu ukweli wote sababu pamekuwepo mengi yaliyosemwa.
RC Makonda alipoanza kujibu swali hilo alisema kuwa suala hilo halihitaji hata mtu awe amekwenda shule badala yake ukitumia tu akili ya kuzaliwa utaweza kupata jibu. Amesema kuwa yeye tangu ameanza kupigania haki za wanyonge kila siku zimekuwa zikiibuliwa kashfa mpya kuhusu yeye.
Hapa chini ni RC Makonda akijibu swali hilo;

0 Responses to “SIKILIZA SAUTI: MAKONDA ALIKIMBIA SWALI LA VYETI ALILOULIZWA NA MWANAFUNZI ”

Post a Comment

More to Read