Friday, March 31, 2017

MWANAMKE AWAGONGA POLISI KWA GARI


gon
Polisi mjini Washington nchini Marekani, wamemfyatulia risasi mwanamke mmoja aliyekuwa ndani ya gari, baada ya kugonga gari la polisi lililokuwa  karibu na Bunge la Marekani na baadaye kujaribu kuwagonga maafisa kadhaa wa polisi.
Tukio hilo lilitokea wakati maafisa wa polisi walipojaribu kumsimamisha dereva huyo mwanamke aliyekuwa akiendesha gari kwa njia isiyo ya kawaida. Ndipo dereva huyo alipogeuza gari kwa haraka nusura awagonge baadhi ya Polisi.
Kwa mujibu wa msemaji wa polisi mjini Washington, Mwanamke huyo hakupigwa risasi lakini alikamatwa na tukio hilo likasababisha kufungwa kwa moja ya majengo ya Bunge.
Mwanamke huyo bado hajatambuliwa wala lengo lake kutambuliwa.
Kisa hicho kinajiri baada ya kushuhudiwa mashambulizi kadha ya watu kugonga wengine kwa magari katika miji ya London na Brussels. Msemaji wa Polisi, Eva Malecki, amesema kuwa mshukiwa ni mwanamke na anatuhumiwa kwa kufanya tukio la uhalifu.
Vikao vya bunge vinaendelea kama kawaida na watalii wameruhusiwa kurudi eneo hilo.

0 Responses to “MWANAMKE AWAGONGA POLISI KWA GARI”

Post a Comment

More to Read