Friday, March 31, 2017
NJIA SITA ZA KUTUMIA MAJI KUJIKINGA NA MAGONJWA MBALIMBALI
Do you like this story?
Watu
wengi wamekuwa wavivu wa kunywa maji, hawajui kuwa maji ni muhimu sana
katika mwili na yanahitajika kwa kiwango kikubwa. Wengi hawajui kuwa
maji ni tiba ya maradhi mengi. Ili maji yawe tiba ya magonjwa, ni lazima
ufuate kanuni ya namna ya kuyatumia.
Maji huwa na faida nyingi. Zifuatazo ni baadhi ya faida za kunywa maji kwa wingi.
Maji husafisha figo. Figo kuwa na uchafu ama vimawe
vidogo vidogo husababishwa na kutokunywa maji ya kutosha. Maji huyeyusha
takataka zote zonazojiunda kutengeneza vijimawe katika mkojo. Hivyo
kunywa maji mengi kutasaidia kusafisha figo zako.
Maji huponya maambukizi ya njia ya mkojo. Kadiri
unavyokunywa maji mengi, ndivyo unavyokojoa zaidi. Kunywa maji kwa wingi
kutasaidia kuondoa bakteria katika kibofu chako cha mkojo.
Maji husaidia kutuliza homa. Homa ni kuongezeka kwa
kiwango cha joto mwilini kinachosababishwa na sababu mbalimbali. Kunywa
maji mengi kutakusaidia kupunguza joto hilo kupitia mkojo. Kama una homa
kunywa maji mengi na utapata ahueni.
Maji husaidia kupunguza uzito wa mwili. Kunywa glasi
moja au mbili muda mchache kabla ya kula kutakufanya ule chakula
kidogo. Kwa vile maji hayana kalori yoyote, itakupunguzia uwezekano wa
kunenepa.
Maji huifanya ngozi yako kuwa laini na nyororo. Maji yatasaidia kuilainisha ngozi yako na kukufanya uwe na macho ang’avu kama tu utayanywa kwa wingi kila siku.
Ushauri wa kiafya wa namna nzuri ya kunywa maji
Kunywa maji punde tu unapoamka. Mwili wako hupoteza
kiwango kikubwa cha maji unapokuwa umelala, hivyo jitahidi kunywa maji
kabla ya kwenda kulala na baada ya kuamka. Unapokunywa maji asubuhi,
husaidia kuondoa sumu zote zilizotengenezwa mwilini ulipokuwa umelala.
Jitahidi kunywa glass 8 mpaka 12 kwa siku. Kulingana
na kliniki ya afya ya Mayo, mtu mwenye uzito wa kilo 55 anatakiwa
kunywa maji glass 8 wakati mtu mwenye uzito wa kilo 87 anatakiwa kunywa
maji glass 12 kwa siku. Inabidi kuhakikisha kuwa rangi ya mkojo inakuwa
nyepesi. Unashauriwa kutokunywa zaidi ya glass 16 kwa siku.
Usisubiri mpaka kiu ikupate ndipo unyewe maji.
Wakati unapohisi kiu, inawezekana umeshapunguza glass 2 katika kiwango
cha maji kinachotakiwa mwilini. Wazee huwa hawapatwi na kiu mara kwa
mara, kwahiyo wanahitajika kunywa maji hata pasipo kuhisi kiu.
Kunywa maji mengi unapokuwa mgonjwa. Hata kama
hujisikii kunywa maji, kiukweli unahitaji kunywa maji zaidi ili
kuusaidia mwili wako kupambana na maradhi. Maji yanapopungua mwilini
mwako, ndivo ugonjwa unavopata nguvu ya kukutesa.
Kunywa maji mengi kama hali ya hewa ni ya joto. Watu
wanaoishi katika maeneo yenye joto kama Dar es salaam, wanatakiwa
kunywa maji kwa wingi. Watu hawa wako katika hatari ya kupata matatizo
ya figo kama hawatakunywa maji kwa wingi ukilinganisga na watu wanaoishi
katika maeneo yenye baridi kama vile Iringa na Mbeya.
Kunywa maji, na siyo vinywaji baridi, vileo ama kahawa. Baadhi
ya wataalamu wanaamini kuwa chai, soda na kahawa vinaweza kuongeza
kiwango cha maji mwilini. Ingawa vinywaji hivyo vina kiwango kikubwa cha
kaboni na sukari ambayo inaweza kuongeza uwezekano wa kupata ugonjwa wa
kisukari na mifupa. Utafiti unaonyesha kuwa watu wanaokunywa vikombe 6
vya kahawa kila siku, huongeza maji mwilini kwa kiwango kidogo sana.
Pombe ndiyo mbaya zaidi kwani hukusababisha ukojoe sana na kupoteza
kiwango kikubwa cha maji mwilini.
Kunywa maji kwa wingi kama unafanya mazoezi. ukiwa unafanya mazoezi,
unatakiwa kunywa maji kwa wingi kwa kuwa unakuwa umepoteza kiwango
kikubwa cha maji mwilini. Ongeza nusu lita zaidi kwa kila nusu saa mpaka
saa moja ya kufanya mazoezi. Kula ndizi kutakusaidia kuongeza kiwango
cha madini ya potassium mwilini.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “NJIA SITA ZA KUTUMIA MAJI KUJIKINGA NA MAGONJWA MBALIMBALI”
Post a Comment