Monday, April 24, 2017
Bila mafunzo hakuna kuendesha bodaboda
Do you like this story?
Ili kukabiliana na ongezeko
la ajali za barabarani, Serikali imewataka madereva wa pikipiki
kuhakikisha wanapata mafunzo kutoka Veta, huku ikiwaonya wamiliki wa
usafiri huo kutowakabidhi madereva ambao hawajapata mafunzo.
Madereva bodaboda
Mkuu
wa Wilaya ya Maswa, Dk Seif Shekalaghe wakati akifunga mafunzo ya
usalama barabara yaliyoandaliwa na serikali ya wilaya hiyo kwa waendesha
pikipiki za kubeba abiria (bodaboda) amesema lengo la mafunzo hayo ni
kuhakikisha ajali za barabarani zinapungua ama kuisha kabisa.
Ameongeza kuwa wamiliki wa bodaboda wanapaswa kutambua kuwa hiyo ni
fursa kiuchumi hivyo ni wajibu wao kuhakikisha kuwa wanawakabidhi
pikipiki watu wenye ujuzi ambao watazilinda dhidi ya uharibifu unaoweza
kusababishwa na ajali zisizo za lazima.
“Wamiliki wa bodaboda mnawekeza fedha nyingi katika kununua bodaboda
lakini wengi wenu mnawakabidhi madereva ambao hawana mafunzo na wanakuwa
chanzo cha ajali za barabarani. Hakikisheni wamepewa mafunzo na ambao
hawana wasaideni wapate ili kuepuka kupoteza pikipiki zenu na nguvu kazi
ya taifa kwa ajali ambazo siyo za lazima"- alisema Dk Seif Shekalaghe.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “Bila mafunzo hakuna kuendesha bodaboda”
Post a Comment