Monday, April 24, 2017
Mwalimu ashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuua
Do you like this story?
Mwalimu
wa Shule ya Msingi Mwamakoye Wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza,
anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumchapa mtoto wake na
kusababisha kifo chake.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema kuwa tukio hilo
lilitokea Aprili 21 mwaka huu, saa kumi jioni na kumtaja marehemu kuwa
ni Sifael Emmanuel (8) mwanafunzi wa shule hiyo.
Aidha,
Msangi amesema kuwa taarifa zilizopatikana zinasema kuwa, mtoto huyo
alikuwa na tabia ya kuchelewa kurudi nyumbani pindi anapoagizwa dukani
na mama yake.
“Kutokana
na tabia hiyo mama yake alikuwa akimpatia adhabu, lakini hakukoma na
kwamba juzi mtoto huyo aliagizwa tena dukani na kuendelea na tabia yake
ile ile ndipo alipoanza kumshushia kipigo hadi kusababishia kifo,”
amesema Msangi.
Ameongeza
kuwa Kutokana na tukio hilo, wananchi walioshuhudia walitoa taarifa
kituo cha polisi na baadaye mwalimu huyo alikamatwa na kupelekwa
kituoni.
Hata
hivyo, Msangi aesema kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika
Hospitali ya Wilaya ya Kwimba kwa ajili ya uchunguzi zaidi na kwamba,
utakapokamilika utakabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya mazishi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “Mwalimu ashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuua”
Post a Comment