Monday, April 24, 2017
Baa la Njaa lanukia Wilayani Wanging'ombe mkoani Njombe
Do you like this story?
Wakazi
wa tarafa ya Wanging'ombe mkoani Njombe wako hatarini kukumbwa na baa
la njaa kutokana na eneo la tarafa hiyo mvua kukatika kabla ya mazao yao
kukomaa kutokana na uharibifu wa mazingira ikiwemo vyanzo vya maji.
Akizungumza
mbele ya kikosi kazi kilichoundwa na Makamu wa raisi Samia Suluhu
Hassani kwaajili ya kuitunza ikojia ya Mto Ruaha Afisa kilimo wa wilaya
hiyo Bernadeta Fivao amesema kuwa licha ya serikali kuzuia wananchi
kulima kwenye vyanzo vya maji kuna uwezekano mkubwa kwa wakulima wa
tarafa hiyo kundelea kulima kwenye vyanzo vya maji kutokana na kukosa
chakula.
Baadhi
ya watumishi wa Halmashauri ya wilaya Wanging'ombe wamekiambia kikosi
kuwa wanasiasa wakiwemo madiwani na wabunge wamekuwa wakihamasisha
wananchi kuendelea kuharibu vyanzo vya maji.
Eneo
la tarafa ya Wanging'ombe limekuwa likikabiliwa na tatizo la uhaba wa
maji kutokana na ufugaji holela pamoja uharibifu wa vyanzo kwa kufanya
kilimo cha mazao kando ya vyanzo vya maji na mito maarufu kama Vinyungu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)