Friday, April 21, 2017
Dawa ya kifafa, hatari kwa wajawazito
Do you like this story?
Utafiti uliofanywa huko
Ufaransa umebaini kuwa dawa ambayo imekuwa ikitumiwa kuwatibu wagonjwa
wa maradhi ya kifafa, zinaweza pia kuathiri afya za watoto wachanga
iwapo wanaotibiwa kwa dawa hizo wako katika umri wa kuweza kupata
watoto.
Idara ya ufaransa inayohusika na viwango vya ubora wa dawa ( National
Agency for the Safety of Medicines) imesema dawa hiyo valproate
imepatikana kusababisha ulemavu wa aina fulani kwa watoto wanne kati
4100 wanaozaliwa ikiwa mama zao walipewa dawa hiyo hasa wakati wa uja
uzito.
Dawa ya valproate ilianza kutumiwa nchini Ufaransa tangu miaka ya 60 na pia ingali inatumika sehemu nyingi duniani .
Sasa madaktari wa Ufaransa wameshauriwa wasiwape dawa hiyo wagonjwa
wajawazito wala wasichana au akina mama walio katika umri wa kujifungua.
Baadhi wa waathiriwa wamesema Sanofi, kampuni wanaotengeza dawa hiyo,
na maafisa wa afya wamejiburuza kuchukua hatua ilhali madhara ya
valproate yalijulikana tangu miaka ya themanini.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “Dawa ya kifafa, hatari kwa wajawazito”
Post a Comment