Saturday, April 22, 2017

Wawili kizimbani kwa kosa la kupigana hadharani


Mahakama ya Wilaya ya Mkokotoni imewaamuru kwenda rumande vijana wawili Abubakar Ramadhan Shaaban (24) mkaazi wa Nungwi na bi Engel Samuel (24) mkaazi wa Nungwi baada ya kushtakiwa kwa kosa la kupigana hadharani.
Imedaiwa na Muendesha Mashtaka khalid Daud mbele ya hakimu muhammed thubeit kwamba siku ya jumatatu ya tarehe 17/ 4 mwakwa huu majira ya saa 11 alfajiri huko Nungwi Wilaya ya Kaskazi A katika baa ya Coco bero watuhumiwa hao walipigana hadharani na kusababishiana majeraha  huku wakijua kwamba jambo hilo ni kosa kisheria.
Mtuhumiwa Abubakar Ramadhan yeye amejeruhiwa kwa kuchinjwa sehemu ya shingoni na miguuni kwa upande wa bi Engel yeye amejeruhiwa kwa kuchinjwa mkono wake wa kulia.
Baada ya kupandishwa mahakamani watuhumiwa hao wote walikataa na kuiomba mahakam iwape dhamana jambo ambalo lilikubaliwa kwa mashariti ya kila mmoja awe na wadhamini 2 na barua za sheha zinazoonesha namba za nyumba na vitambulisho vya mzanzibari masharti ambayo yaliwashinda.
hivyo mahakama hiyo imewarudisha rumande watuhumiwa hao na kusubiri  hadi tarehe 24 mwezi huu kesi yao itakapotajwa tena.

0 Responses to “Wawili kizimbani kwa kosa la kupigana hadharani ”

Post a Comment

More to Read