Saturday, April 22, 2017
Afariki Dunia kwa kutumbukia kisimani
Do you like this story?
Mtu
mmoja ambae ni mgonjwa wa akili amefariki Dunia baada ya kutumbukia
ndani ya kisima kilichopo maeneo ya Sokoni mzuri Makunduchi.
Kwa
mujibu wa taarifa zilizosibitiswa na kaimu kamanda wa Mkoa wa Kusini
Unguja, Kamishna Msaidizi wa Polisi Kheri Mussa kuwa marehe huyo
aliyejulika kwa jina la Wanu Ameir Chum ambapo tukio hilo limetokea jana
huko Mzuri Makunduchi.
Aidha
Kamanda huyo alitoa wito wa watu wanaoishi na wagonjwa wa akili kuwa
karibu nao na kutowaacha peke yao majumbani ili kuweza kuepusha majanga
kama hayo.
Mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi katika Hospitali ya Koteji Makunduchi na kukabidhiwa kwa jamaa zake kwa ajili ya mazishi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)