Thursday, April 13, 2017
HAKUNA UPUNGUFU WA ARV's TANZANIA..KIWANDA CHA KUZALISHA ARV's KUJENGWA ARUSHA
Do you like this story?
BUNGE limearifiwa kuwa kwa sasa nchi haina tatizo la upungufu wa dawa za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi (ARVs).
Kauli hiyo ilitolewa bungeni na Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Fatma Toufiq (CCM)
aliyetaka kufahamu mpango wa serikali wa kuwa na kiwanda cha kutengeneza
ARVs.
Waziri Ummy alisema kuhusu dawa za ARVs
zinazoingizwa nchini, kuna dawa za watoto ambazo ni pamoja na Nevirapine
Syrup na Lopinavir/Ritonavir Syrup.
Alisema dawa nyingine ni pamoja na
mchanganyiko wa dawa za vidonge mfano Lamivudine/Atazanavir/ Niveraphine
(3TC/AZT/ NPV) zenye nguvu ya 30mg/60mg.
Alisema serikali inahamasisha mashirika,
taasisi, wafanyabiashara wakubwa na wawekezaji kuwekeza kwenye viwanda
vya kuzalisha dawa mbalimbali zikiwemo ARVs.
Alisema kwa sasa kuna kiwanda mkoani Arusha cha TPI ARV Limited ambacho kimepewa leseni ya kutengeneza ARVs.
“Kiwanda hakijaanza uzalishaji, wizara inatarajia kiwanda hicho kitaanza uzalishaji wa ARVs hivi karibuni,” alisema Waziri Ummy.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “HAKUNA UPUNGUFU WA ARV's TANZANIA..KIWANDA CHA KUZALISHA ARV's KUJENGWA ARUSHA”
Post a Comment