Thursday, April 13, 2017

MKUU WA MKOA AINGILIA KATI MGOGORO WA WAPI KUWE MAKAO MAKUU YA KATA YA SHIZUVI MBEYA


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Mkalla akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Inyala Ilembo kilichopo Mbeya Vijijini kumaliza Mgogoro uliodumu kwa muda Mrefu(Picha na David Nyembe wa Fahari News Mbeya)

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Mkalla akiwasili katika kijiji cha Shizuvi Mbeya Vijijini



Wananchi wakishangilia uwamuzi wa Mkuu wa Mkoa





 Mkuu wa Mkoa Afanya mkutano Kijiji cha Inyala ilembo ukishirikisha Vijiji vya Shisyete na Isonzo Vijiji 3 vinavyounda kata ya Shizuvi.

Hata hivyo  Baada ya kusikiliza pande zote Mkuu wa Mkoa amesitisha zoezi lote la kuhamisha makao makuu Baada ya kubaini kuwa wananchi hawakushirikishwa kikamilifu
 Aagiza watendaji waendelee kufanya kazi za kata Kijiji cha Inyala Ilembo

Amesema  Ataunda Kamati itakayoratibu maoni ya wananchi na wataamua wananchi ni wapi pawe makao makuu ya Kata
Ameshangaa kuona uamuzi ulivyofanywa kwa usiri bila kushirikisha wananchi.

kwa Upande wa Wananchi wamefurahishwa uamuzi wa kusitisha zoezi la kuhamisha makao makuu Kata.
Pia Wananchi wa Kijiji cha Inyala ilembo wamtuhumu Diwani kuhamisha makao makuu ya  kata kutoka Kijiji cha Inyala- Ilembo kwenda Kijiji Shisyete

0 Responses to “MKUU WA MKOA AINGILIA KATI MGOGORO WA WAPI KUWE MAKAO MAKUU YA KATA YA SHIZUVI MBEYA ”

Post a Comment

More to Read