Tuesday, April 18, 2017
Kijana wa miaka 22 afariki dunia baada ya kuzama mtoni
Do you like this story?
Kijana
mmoja anaetambulika kwa Jina la Suleiman Mtumwa Suleiman mwenye umri
wa miaka 22 amefariki dunia baada ya kuzama katika Mto wa Faki Abuu
hapo jana huko kilombero Wilaya ya kaskazini B.
Wakizungumza
na mwanahabari wetu baadhi ya mashuhuda katika tukio hilo Hija Ali Hija
na Habiba Mohamed wamesema tukio hilo limetoka jana majira ya saa 11
jioni na jitihada za uwokozi zilifanyika lakini alishindikana kupatikana
hadi leo baada ya kikosi cha uwokozi kufika katika tukio hilo.
Kwaupande
wake Daktari wazamu wa Hospitali ya Kivunge Makame Mdungi Makame
amethibitisha kupokea mwili wa kijana huyo aliyefariki dunia baada ya
kuzama katika mto, huko kilombero na amesema kifo chake kimesababishwa
na kunywa maji mengi katika mto huo.
Aidha
Daktari huyo alitoa wito kwa wananchi kuchukua tahadhari kwa
kuwadhibiti watoto wao kucheza karibu na mito na maeneo yaliyotuama
maji ili kuepukana na majanga yanayoweza kujitokeza.
Matukio ya kuzama kwa watoto katika kijiji cha kilombero hutokea mara kwa mara hususani kipindi kama hichi cha mvua.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)