Tuesday, April 18, 2017
Muumini akamatwa akiiba sadaka kanisani
Do you like this story?
Muumini
mmmoja wa Kanisa la EAGT Jerusalem Kata ya Majengo, Wilaya ya Kahama
mkoani Shinyanga amekamatwa na waumini wenzake kwa madai ya kuiba sadaka
wakati wakiwa katika maombi.
Tukio
hilo lilitokea Jumapili iliyopita Aprili 9 saa 11 jioni wakati
Mchungaji Felix Gwamiye, akiongoza maombi huku waumini wakiwa wamefumba
macho na mtuhumiwa huyo alijifanya anatoa sadaka na kuchota sh. 20,000
ndani ya sanduku.
Mmoja
wa waumini wa kanisa hilo ambaye hakutaka jina lake kutajwa alisema
licha ya muumini huyo kuondoka kiasi hicho, siku hiyo hiyo misa ya
asubuhi alidakwa na Mashemasi wa kanisa hilo akichukua fedha
isiyofahamika wakati alipoungana na waumini wengine kwenda kutoa sadaka,
hata hivyo alisamehewa.
Mchungaji
Gwamiye alithibitisha kutokea kwa tukio hilo kanisani kwake na kusema
kwamba kumekuwepo na wimbi la vibaka wanaoingia ndani ya makanisa wakati
maombi yakiendelea na kudokoa fedha za sadaka.
Katika
tukio hilo Mchungaji Gwamiye alitoa wito kwa Makanisa ya Kipentekoste
wilayani Kahama kukaa chonjo na vibaka wanaoingia makanisani na
kujifanya ni waumini huku lengo lao likiwa ni kuvizia sadaka za waumini.
“Mtuhumiwa
huyo alikamatwa na Mashemasi wakati walipomuona akiiba hela za sadaka
baada ya kuanza maombi. Kama kiongozi wa kanisa hili nimemsamehe, lakini
asithubutu kuingia katika makanisa yoyote hapa kahama maana waumini
wakiamua kufunga novena ya maombi laana itamsumbua” alisema Gwamiye
Hata
hivyo muumini huyo aliyejulikana kwa jina Dismas Simon mwenye umri wa
miaka 35 alisema kuwa shetani ndiye aliyemtuma na kujikuta anaondoka na
kiasi hicho cha fedha. Alimuahidi kiongozi huyo wa kanisa kuteua watu wa
kuongozana nao kwa ndugu yake hali ambayo ilimfanya mchungaji amsamehe
Subscribe to:
Post Comments (Atom)