Tuesday, April 18, 2017
Mke wa Roma Mkatoliki Aibua mwengine kuhusu mume wake kutekwa
Do you like this story?
Mke
wa msanii Roma Mkatoliki, Nancy Mshana amefunguka kwa mara ya kwanza
toka mume wake alipotekwa na kupatikana na kuwashukuru Watanzania ambao
walikuwa pamoja na yeye katika kipindi kigumu.
Mrembo
huyo ametumia maneno ya kwenye Biblia kutoka katika kitabu cha Yeremia
kufikisha ujumbe wake kwa watu ambao wamemfanyia ubaya mume wake na
kusema kuwa na wao watakutwa na mabaya hayo.
“(Yeremia
30:16-17) Basi, watu wote wakulao wataliwa; na adui zako wote
watakwenda kufungwa; kila mmoja wao; na hao waliokuteka nyara watatekwa;
na wote waliokuwinda nitawafanya kuwa mawindo. Maana nitakurudishia
afya, nami nitakuponya jeraha zako, asema Bwana.Ameen” Alinukuu mke wa
Roma Mkatoliki.
Mbali na hilo Nancy alitumia nafasi hiyo kuwashukuru wote ambao wamesimama na wao katika kipindi hiki kigumu.
“Ahsanteni wote mliosimama na sisi katika kipindi kigumu tulichopitia !! Mungu awabariki sana” aliandika Nancy.
Msanii
Roma Mkatoliki bado anaendelea na matibabu kufuatia tukio lake la
kutekwa na kuumizwa katika sehemu mbalimbali za mwili wake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)