Tuesday, April 18, 2017

Flaviana Matata Kweli ni Matata, Ajiachia na Wiz Khalifa, Rihanna, Keri Hilson


Mwanamitindo wa Tanzania, Flaviana Matata akiwa na Wiz Khalifa.
Mwanamitindo wa Tanzania, kupitia ukurasa wake wa Twitter, ametupia picha na video mbalimbali akiwa na mastaa wa Marekani.
Flaviana Matata ambaye amekuwa akifanya kazi zake nyingi nje ya Tanzania, aliweka picha akiwa na mwanamuziki Wiz Khalifa wa Marekani kisha kuandika: “It has been a fun weekend, more on my Snapchat and IG stories”

Aidha, Flaviana pia aliweka picha akiwa na staa wmingine wa R&B na Pop wa Marekani, Keri Hilson kisha akaweka video akidansi huku pembeni yake akiwepo Rihanna na kueleza jinsi ambavyo anavyomkubali mwanamuziki huyo ambaye licha ya kuwa ni staa lakini aliamua kujichanganya na watu wa kawaida kwenye tamasha fulani ambalo hakifafanua.

0 Responses to “Flaviana Matata Kweli ni Matata, Ajiachia na Wiz Khalifa, Rihanna, Keri Hilson ”

Post a Comment

More to Read