Thursday, April 27, 2017

Staa wa soka England amefungiwa miezi 18 kwa sababu ya Betting


Betting ni miongoni mwa michezo inayochukua headlines katika soka kwa siku za hivi, imekuwa ni kawaida kuwaona mashabiki wa soka mbalimbali wakijihusisha na betting, headlines za mchezo wa betting leo zimemgusa staa wa soka wa Burnley Joe Barton.
Staa wa soka wa Burnley aliyewahi kuvichezea vilabu mbalimbali vya Ligi Kuu England Joe Barton amefungiwa miezi 18 kujihusisha na soka kutokana na kujihusisha na mchezo wa betting ambapo kwa mujibu wa kazi yake ni kosa kwa sheria za chama cha soka England FA.
Barton
Barton mwenye umri wa miaka 34 amepigwa faini ya pound 30000 na adhabu ya kufungiwa miezi 18 baada ya kuvunja sheria za FA na kujihusisha na betting, Barton alifanya kosa hilo kuanzia March 26 2006-May 13 2016.
Joe Barton ambaye anajiandaa kukata rufaa kutokana na adhabu hiyo kuwa ndefu amekiri kuwa yuko addicted na Betting na atakata rufaa kwa kupeleka FA ripoti ya daktari, Barton pia ameripotiwa kuwahi ku-bet moja kati ya mechi alizocheza kitu ambacho ni kosa na inadaiwa kupelekea upangaji wa matokeo.

0 Responses to “Staa wa soka England amefungiwa miezi 18 kwa sababu ya Betting”

Post a Comment

More to Read