Thursday, April 27, 2017

Ushindi wa 7-1 wa Barcelona umeishusha daraja Osasuna, Real akipata ushindi wa 6-2


Baada ya kumalizika kwa mchezo wa El Clasico April 23 kati ya Real Madrid waliyowakaribisha wapinzani wao wa jadi FC Barcelona katika uwanja wao wa Santiago Bernabeu na Madrid kupoteza kwa magoli 3-2, usiku wa April 26 Real Madrid walikuwa ugenini kuwakabili Deportivo wakati Barcelona wakiikaribisha Osasuna katika uwanja wa Nou Camp.

Kwa sasa Real Madrid na Barcelona wote wana point 78 wakitofautiana magoli ya kufunga na kufungwa huku Barcelona akiizidi mchezo mmoja Real Madrid, hivyo ushindi wa Barcelona wa magoli 3-2 wa El Clasico umeifanya timu hiyo kulazimika kufunga magoli mengi katika kila mchezo ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutwaa LaLiga hata kwa tofauti ya magoli.
Baada ya ushindi wa magoli 7-1 dhidi ya Osasuna Barcelona imekuwa timu ya kwanza msimu huu katika Ligi 5 kubwa Ulaya kufunga magoli zaidi ya 100+ msimu huu
Barcelona akiwa nyumbani amefanikiwa kupata ushindi wa magoli 7-1 dhidi ya Osasuna na kuishusha daraja timu kutokana na Leganes wamepata ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Las Palmas, hivyo rasmi Osasuna wanacheza michezo ya kukamilisha ratiba LaLiga na wanasubiri kucheza Segunda msimu ujao.
Javier Mascherano akifurahia goli lake la kwanza katika maisha yake Barcelona toka alipojiunga nayo 2010 akitokea Liverpool ya England amecheza jumla ya mechi 319.
Real Madrid wao wakiwa ugenini dhidi ya Deportivo La Coruna katika uwanja wa Riazor wamefanikiwa kupata ushindi wa magoli 6-2, licha ya kuwakosa wachezaji wao nyota kama Toni Kroos na Ronaldo waliyopumzishwa, nahodha wao Sergio Ramos anayetumikia adhabu ya kadi nyekundu ya El Clasico na Gareth Bale ambaye atakuwa nje ya uwanja kwa wiki tatu kwa kuwa na majeruhi.
Msimamo wa LaLiga baada ya matokeo ya mechi za April 26 2017

0 Responses to “Ushindi wa 7-1 wa Barcelona umeishusha daraja Osasuna, Real akipata ushindi wa 6-2”

Post a Comment

More to Read