Friday, April 7, 2017
Waziri mkuu nchini DRC ajiuzulu
Do you like this story?
Waziri mkuu nchini
Jamhuri ya Demokrasi ya Congo Samy Badibanga amejiuzulu kama sehemu ya
makubaliano yaliyoongozwa na kanisa katoliki kumaliza mzozo wa kisiasa
nchini humo, kwa mujibu wa Redio moja ya nchi hiyo, Redio Okapi.
Hii
inafuatia hotuba ya hapo jana kutoka na Rais Joseph Kabila, ambapo
aliwaambia wabunge kuwa atamteua waziri mkuu kutoka upinzani ndani ya
saa 48 zinazokuja.
Bwana Kabila alisema kuwa atafuata tararibu
zilizoafikiwa kama sehemu ya makubaliano na upinzani ambayo yanataka
uchaguzi kuandaliwa kabla ya mwisho wa mwaka huu.
Kumekuwa na msukosuko nchini DRC baada ya Kabila kukataa kundoka madarakani wakati muhula wake ulipokamilika mwezi Disemba.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “Waziri mkuu nchini DRC ajiuzulu”
Post a Comment