Wednesday, May 3, 2017

Mrisho Mpoto afunguka baada ya kutukanwa kwa madai ya kusema ‘Rais Magufuli ni Mungu’


Mwanamuziki wa nyimbo za miondoko ya asili, Mrisho Mpoto ameonyesha kusikitishwa kwake na baadhi ya watu kumtukana baada ya yeye kuonyesha kumuunga mkono Rais Dkt Magufuli.
Mpoto amesema kuwa sababu kubwa iliyopelekea yeye kutukanwa ni maneno ya uongo yaliyozushwa mitaani kuwa amesema ‘Rais Magufuli ni Mungu.
Kufuatia madai hayo, Mpoto ameandika ujumbe huu kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Nimepokea matusi mengi, kebehi, na maneno machafu juu ya mimi kuunga mkono utendaji wa Rais Magufuli, kitu ambacho nakiamini kuna “KUKUBALIANA KWA KUTOKUBALINA” lakini siyo kumtukana mtu mwingine siyo busara hata kidogo, kwakua tu hakusema au hakufanya ambacho nafsi yako ilipenda kusikia.
Kilichonifanya niandike ujumbe huu ni kuwa nisiwekewe maneno mdomoni yakua nimesema Rais Magufuli ni Mungu, kwa wale ambao hawakuangalia sherehe za MEI MOSI jana, naomba niseme kuwa hayo maneno siyo kweli na yamebadilishwa kutoka kwenye ukweli wa niliosema.
Mimi ni mtu mwenye hofu na Mungu siwezi kusema hivyo, kumekuwa na utamaduni ikitokea mtu anauunga mkono utendaji wa Rais kuna ibukuka kundi la wapinga Maendeleo na kuanza kutukana. Naomba ijulikane kuwa sababu za kumunga mkono Rais, yale niliyokua nayaongea huko nyuma naona yanafanyiwa kazi hivi sasa!!
MRISHO MPOTO mpaka sasa namuunga mkono Rais MAGUFULI, Iwe nachumia tumbo kama inavyosemwa au nimevimbilwa kwa shibe.

0 Responses to “Mrisho Mpoto afunguka baada ya kutukanwa kwa madai ya kusema ‘Rais Magufuli ni Mungu’”

Post a Comment

More to Read