Thursday, June 12, 2014

12 Jun 2014 MOTO WATEKETEZA SOKO LA MITUMBA LA KARUME JIJINI DAR JANA USIKU





Pichani ni mwanga wa moto unaotoka ndani ya soko la mitumba la Karume lililopo maeneo ya Ilala jirani na Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es salaam  ambalo linateketea na moto usiku WA JANA.

Taarifa zilizotufikia katika meza ya habari usiku WA JANA zinasema kuwa moto huo ulianza kidogo kidogo katika baadhi ya vibanda ambavyo wenye navyo walikuwa hawapo, kabla ya kushika  kasi na kuteketeza kila kitu kilichopo kwenye eneo  hilo.

0 Responses to “ 12 Jun 2014 MOTO WATEKETEZA SOKO LA MITUMBA LA KARUME JIJINI DAR JANA USIKU ”

Post a Comment

More to Read