Wednesday, September 10, 2014

UZINDUZI WA KIVUKO CHA MV KIGAMBONI.

Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akiongea na wajumbe mbalimbali waliofika katika uzinduzi wa kivuko cha kigamboni leo jijini Dar es Salaam kinachofanyiwa matenganezo na Jeshi la Wanamaji maeneo ya kurasini ,ambacho kinatarajiwa kuanza kutumika rasmi alhamisi wiki hii.

Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli ( kushoto) na Katibu Mkuu wa Ujenzi Injinia Mussa Iyombe(kulia) wakisikiliza kwa makini maelekezo yaliyokuwa yakitolewa katika ufunguzi wa kivuko cha Mv Kigamboni leo jijini Dar es Salaam kinachofanyiwa matenganezo na Jeshi la Wanamaji maeneo ya kurasini na kinatarajiwa kuanza kutumika wiki hii.

Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli ( katikati) akipata maelekezo kutoka kwa Msimamizi wa matengenezo Luten Kanali Abel Gwanafyo (Kushoto), kulia ni Mkuu wa Jeshi nla Maji Brigadia Jenerali Rostian Laswai wakati wa ufunguzi wa kivuko hicho leo jijini Dar es Salaam ,amabapo kinatarajiwa kuanza kutumika wiki hii kurahisisha usafiri kwa watu wa Kigamboni.

Kivuko cha Mv Kigamboni kinavyoonekana upande wa mbele na ubavuni , kikiwa katika hatua za mwisho tayari kwa kuanza kutumiwa na wananchi siku ya alhamisi baada ya matengenezo yaliofanywa na Jeshi la Wanamaji kwa mda wa wiki tatu tangu kilipoaacha kufanya kazi Agosti 14 mwaka huu.( Picha na Lorietha Laurenc eMaelezo)

0 Responses to “UZINDUZI WA KIVUKO CHA MV KIGAMBONI.”

Post a Comment

More to Read