Thursday, October 9, 2014
MAITI YAKAA MOCHWARI SIKU 34, KISA MGOGORO WA WAZAZI.
Do you like this story?
Moshi. Mgogoro
mwingine mkubwa wa kifamilia wa kugombea maiti, umeibuka mjini Moshi na
kusababisha mwili wa Rosemary Marandu (38), kuhifadhiwa mochwari kwa siku 34.
Mwili wa marehemu
huyo aliyefariki dunia Septemba 4, mwaka huu umehifadhiwa katika Hospitali ya
Rufaa ya KCMC na umekuwa ukilipiwa Sh9,000 kwa siku, hivyo siku 34 gharama yake
imefikia Sh306,000.
Tukio hilo limekuwa
gumzo mjini Moshi hasa baada ya kutokea siku chache baada ya maiti nyingine ya
Steven Assey kufukuliwa kwa amri ya Mahakama na hadi leo ni siku ya 29 bado
haijazikwa licha ya mke mdogo wa marehemu, Fortunata Lyimo kupewa haki ya
kuzika lakini amekataa akisema ni kinyume cha mila na utamaduni wao kwa mtu
kuzikwa mara mbili. Akizungumza jana, mama mzazi wa Rosemary Marandu, Felicia
Nkya, alidai kuwa mumewe aitwaye Flavian Marandu ndiye anayeshikilia mwili huo
hadi leo.
Marandu ni Diwani wa
Kata ya Mrao Keryo kwa tiketi ya CCM na anamiliki vitega uchumi kadhaa vikiwamo
viwanda vya kupasua mbao na nyumba za kulala wageni.
“Ukweli ni kwamba
tangu amekufa (Marandu) hajatupa taarifa yoyote zaidi ya kunitumia meseji ya
simu akiniuliza kama mume wa Rosemary ameniambia kama Rosemary amekufa. Kwa
mila na utamaduni wetu, mtu akifa tunakaa pamoja na kupanga mazishi lakini hadi
leo hajatuma mtu yeyote kuzungumza na sisi juu ya msiba.”
Felicia alisema
walitengana na mumewe huyo mwaka 1982 na mtoto wao huyo amezaa watoto wanane na
wanaume tofautitofauti na mumewe aliyemfia, Sigfrid Mlingi naye amezuiwa
kumzika.
“Naumia sana napata
mateso makubwa ya kiakili na kisaikolojia. Mwezi mzima sasa sijui hatima ya
mazishi ya mtoto wangu. Hakuna chakula kinachopita naomba mnisaidie jamani,”
alilalamika.
Mama huyo alidai kuwa
awali walikwenda kulalamika polisi ambako walishauriwa kufungua shauri
mahakamani lakini akadai kwamba hawana nguvu ya kushindana na Marandu.
“Tumeamua kumkabidhi
Mungu kwa sababu hatuwezi kushindana naye (Marandu) tukamshinda. Hata kule KCMC
anadai kuna kesi mahakamani lakini sisi hatujafungua kesi,” alidai.
Mumewe azungumza
Mlingi alisema
ameamua kujiweka kando kushughulikia mazishi ya mkewe baada ya baba mkwe
kumtolea lugha isiyofaa.
“Mimi ndiye
nilimuuguza hapo Mawenzi mpaka akanifia mikononi mwangu na baada ya kufa
nilikwenda Keryo na kuonana na baba yake lakini akanifukuza,” alidai Mlingi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


.gif)


0 Responses to “MAITI YAKAA MOCHWARI SIKU 34, KISA MGOGORO WA WAZAZI.”
Post a Comment