Monday, November 17, 2014

HATARI TENA.....RAIA HUYU WA MAREKANI AKATWA KICHWA NA KUNDI LA IS.


Peter Kassig enzi za uhai wake.



Kanda moja ya video iliowekwa mtandaoni inaonyesha mauaji ya mtu wa kutoa huduma za misaada raia wa Marekani Abdul Rahman Kassig ambaye alikuwa anajulikana kama Peter Kassig kabla ya kutekwa nyara na wanamgambo wa Islamic State nchini Syria mwaka uliopitaVideo hiyo inamuonyesha mwanaume mmoja anayeonekana kuwa mwanachama wa Islamic State akiwa na kisu mkononi na maandishi yanayosema kuwa Peter Kassig ameuawa.

Kanda hiyo pia ina picha za watu kadha waliouawa ambao wanasemekana kuwa wanajeshi wa Syria waliokuwa wametekwa nyara.Marekani imesema kuwa inafanya juhudi za kubaini chimbuko la kanda hiyo.

Bwana Kassig ambaye anajulikana kama Peter alitekwa nyara mwaka uliopita.Mnamo mwezi Octoba kanda nyengine ya video ya kifo cha mfanyikazi mwengine wa misaada kutoka Uingereza Alan Henning iliisha huku Kassig akitishiwa.
(Chanzo: BBC)

0 Responses to “HATARI TENA.....RAIA HUYU WA MAREKANI AKATWA KICHWA NA KUNDI LA IS.”

Post a Comment

More to Read