Thursday, November 13, 2014

KAMA ULIKUWA HUJUI WA NDIO MARAIS WALIOUAWA KWA KUPIGWA RISASI




BAADA
ya wiki iliyopita kuwaletea marais wa Afrika waliofia madarakani. Yaani
walikuwa wakiongoza nchi zao wakakumbwa na mauti. Wiki hii tunawaletea
marais waliouawa kwa kupigwa risasi wakiwa madarakani.

ABRAHAM
Lincoln; alikuwa Rais wa 16 wa Marekani. Aliuawa mwaka 1865 jijini
Washington kwa kupigwa risasi kichwani kwa nyuma na John Wilkes. Alikuwa
amekaa na mkewe. Bastola iliyotumika inaitwa Deringer.

INDIRA
Priyadarshini Gandhi; alikuwa Rais wa India. Aliuawa mwaka1984 kwa
kupigwa risasi na walinzi wake, Satwant Singh na Beant Singh jijini New
Delh, India.

JOHN Francis Kennedy ‘JFK’; ni Rais wa 35 wa Marekani.
Aliuawa mwaka 1963 mjini Dallas kwa kupigwa risasi na Lee Harvey akiwa
kwenye gari la wazi barabarani.

LAURENT Desire Kabila;
alimng’oa madarakani Rais Mabotu Seseko wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya
Kongo, lakini mwaka 2001 akauawa kwa kupigwa risasi na watu
wanaosadikiwa ni walinzi wake.

THOMAS Isdor Noel Sankara; alikuwa
Rais wa Burkina Faso Alitawala nchi kwa miaka 4 hadi 1984 alipouawa kwa
kupigwa risasi na Blaise Compaore ambaye hivi karibuni ameikimbia nchi
hiyo. 

WILLIAM Richard Tolbert Jr; alipigwa risasi mwaka 1980
katika mapinduzi ya kijeshi akiwa Rais wa Liberia. Samuel Doe akiwa na
cheo cha sajenti ndiye aliyetajwa kumuua.


MUHAMMAR Muhamad Abu
Migar al Ghaddaf; alikuwa Rais wa Libya kwa miaka 42. Aliuawa kwa
kupigwa risasi ya kichwa kwenye vurugu za kisiasa mjini Sirte, Libya,
Oktoba 20, 2011.

ABEID Amani Karume; alikuwa Rais wa Zanzibar tangu
mapinduzi ya mwaka 1964. Aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa anacheza bao
mwaka 1972 na mtu ambaye hakuwahi kupatikana.

Jean baptist
ouedraogo; aliitawala Burkina Faso kwa mwaka mmoja tu, 1982-83. Aliuawa
kwa kupigwa risasi na Thomas Sankara ambaye alichukua madaraka ya
kuiongoza nchi hiyo kabla na yeye kupinduliwa.

0 Responses to “KAMA ULIKUWA HUJUI WA NDIO MARAIS WALIOUAWA KWA KUPIGWA RISASI”

Post a Comment

More to Read