Wednesday, November 26, 2014
MWAKYEMBE AKABIDHIWA RIPOTI YA AJALI ZA BARABARANI
Do you like this story?
Waziri wa Uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe
amekabidhiwa Ripoti ya kamati iliyoundwa kutathmini na kutoa mapendekezo hatua
ya kuchukua ili kupunguza ajali za barabarani.
Kamati hiyo iliyoundwa na watu 14 imebaini changamoto
zinazopelekea ajali hizo kuwa ni pamoja na ratiba za mabasi zinazotolewa na
SUMATRA kutozingatiwa pamoja na utaratibu mbovu wa utoaji wa leseni.
Akizungumza wakati wa kupokea Ripoti hiyo Mwakyembe
amesema; “… Ajali nchini zinasababishwa na Mwendokasi na uendeshaji hatarishi
au kwa maneno mengine uzembe. Waziri Gaudensia Kabaka yeye tayari Wizara yake
imefanya kazi kubwa kweli, wamekuja wao na ratiba kabisa ya ukaguzi wa kampuni
zote za mabasi na malori, ni ratiba ya miezi miwili kuchunguza mikataba ya kazi
kwa upande wa madereva kwa mwezi Desemba na Januari, inasubiri tu Waziri aseme
tunaanza tarehe fulani.
Kwa hiyo siyo tu mikataba ya kazi inaangaliwa,
itaangaliwa mpaka na michango ya mwajiri au waajiri na waajiriwa kwenda kwenye
mifuko ya Hifadhi ya Jamii…”– Mwakyembe.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MWAKYEMBE AKABIDHIWA RIPOTI YA AJALI ZA BARABARANI”
Post a Comment