Monday, November 17, 2014
TFF YAIPONGEZA AFRIKA KUSINI KWA KUFUZU AFCON.
Do you like this story?
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) limetoa pongezi kwa Chama cha Mpira wa Miguu Afrika Kusini (SAFA)
kufuatia timu yake ya Taifa (Bafana Bafana) kufuzu kucheza fainali zijazo za
AFCON nchini Equatorial Guinea.
Afrika Kusini iliifunga Sudan mabao 2-1,
hivyo kufuzu kabla ya kukamilisha michezo yote. Bafana Bafana bado imebakiza
mchezo mmoja katika hatua hiyo.
Wakati huo huo, TFF imeipeleka barua ya
shukrani kwa Chama cha Mpira wa Miguu Afrika Kusini (SAFA) kwa kufanikisha
kambi ya Taifa Stars nchini humo kabla ya kwenda kucheza Swaziland.
SAFA ilitoa viwanja vya mazoezi kwa Taifa
Stars na usafiri wa basi la kisasa kutoka Johannesburg kwenda Swaziland na
kurudi, hivyo kuokoa zaidi ya dola 15,000 ambazo TFF ingetumia kama
ingegharamia yenyewe safari hiyo au kuweka kambi ya timu hiyo nyumbani.
Awali Benchi la Ufundi la Taifa Stars
chini ya Kocha Mart Nooij lilipendekeza timu kufika Swaziland mapema au kuweka
kambi nchini Afrika Kusini. SAFA ikajitolea kusaidia kambi hiyo.
Pia TFF inakanusha madai ya gazeti moja la
kila siku lililodai kuwa wakaguzi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL)
wamevamia/wamefanya ukaguzi wa siri kukagua fedha za udhamini wao kwa Taifa
Stars.
Ukaguzi wa hesabu ni utaratibu wa kawaida
wa kila robo ya mwaka wa fedha. TFF ndiyo huwaalika TBL kutuma wakaguzi wao ili
kuhakiki vitabu vya fedha. Uhusiano kati ya TFF na TBL ni mzuri, na kila
kinachofanyika ni kwa nia njema kwa makubaliano ya pande zote mbili.
IMETOLEWA
NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TFF YAIPONGEZA AFRIKA KUSINI KWA KUFUZU AFCON.”
Post a Comment